Exodus 30:22-27

22 aKisha Bwana akamwambia Musa, 23 b“Chukua vikolezi bora vifuatavyo: shekeli 500
Shekeli 500 ni sawa na kilo 6.
za manemane ya maji, shekeli 250
Shekeli 250 ni sawa na kilo 3.
za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli 250 za miwa yenye harufu nzuri,
24 eshekeli 500 za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hini
Hini moja ni sawa na lita 4.
ya mafuta ya zeituni.
25 gVitengeneze vikolezi hivi kuwa mafuta matakatifu ya upako yenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Yatakuwa mafuta matakatifu ya upako. 26 hKisha yatumie kupaka hilo Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda, 27meza na vifaa vyake vyote, kinara cha taa na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba,
Copyright information for SwhKC